Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Thomas Tuchel, amesema kuwa nafasi ya kiungo mshambuliaji Phil Foden katika kikosi cha Kombe la Dunia si ya uhakika kutokana na kushindwa kuonesha kiwango chake bora mara kwa mara akiwa na timu hiyo.
Foden alipata wakati mgumu katika mchezo wa kirafiki ambao England walipoteza kwa mabao 1-0 dhidi ya Japan, ambapo alicheza nafasi isiyo ya kawaida ya ushambuliaji kufuatia kutokuwepo kwa mshambuliaji Harry Kane.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Licha ya kuanza msimu kwa kiwango kizuri, nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amepoteza nafasi ya kudumu katika kikosi cha Manchester City kinachonolewa na Pep Guardiola katika wiki za hivi karibuni.
Akizungumzia hali ya Foden, Tuchel alisema “Alijitahidi kwa kila hali. Ningesema alikuwa bora sana kambini, lakini bado anapata ugumu kuonesha hilo uwanjani.”
Aliongeza kuwa “Hakupata muda mwingi wa kucheza akiwa Manchester City hivi karibuni, lakini alipokuja kambini alikuwa na ari kubwa na alifanya vizuri mazoezini. Tulidhani angekuja kutushangaza kwa kiwango kilekile, lakini ameshindwa kuwa na athari kubwa uwanjani.”
Foden anakabiliwa na ushindani mkali katika nafasi ya kiungo mshambuliaji kutoka kwa wachezaji wenzake akiwemo Jude Bellingham, Cole Palmer na Morgan Rogers, hali inayofanya nafasi yake kuwa shakani zaidi kuelekea michuano hiyo.
Kuhusu uwezekano wa kumjumuisha Foden katika kikosi cha mwisho, Tuchel alisema “Sio uhakika kwamba ataenda. Hatuwezi kuchukua mchezaji ambaye yuko katika kiwango cha chini kwenda fainali.”
Licha ya kipigo dhidi ya Japan kuwa cha pili kwake katika michezo 12 tangu awe kocha wa England, Tuchel bado hajaifunga timu yoyote iliyo katika 20 bora za viwango vya FIFA tangu aanze kazi hiyo.
Hata hivyo, baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Uruguay, kocha huyo ameonesha matumaini kuwa matokeo ya mwezi Machi hayataathiri malengo yao ya muda mrefu.
Akihitimisha, Tuchel alisema “Hatutakata tamaa ya ndoto yetu. Jambo muhimu sasa ni wachezaji kurejea katika vilabu vyao, kumaliza msimu vizuri, kisha tujiandae ipasavyo kwa hatua zinazofuata.”


