Kocha mkuu wa Bayern Munich Hansi Flick anasema anaweza kuelewa kwanini nyota anayetajwa kufukuziwa na Liverpool, Thiago Alcantara anataka Ligi Kuu.

Mkataba wa Thiago unaisha mwaka ujao na tayari mwenyekiti wa Bayern bwana Karl-Heinz Rummenigge alithibitisha mwezi uliopita kuwa kiungo huyo atawaacha mabingwa hawa wa Bundesliga.

Liverpool ndiye anayetajwa kuiwania saini ya staa huyu wa zamani wa Barcelona, ​​wakati Paris Saint-Germain pia wakihusishwa na staa huyu wa Uhispania.

Bosi wa Bayern Flick alieleza kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa anataka kuhamia Uingereza, akionesha masikitiko yake juu ya staa huyu mwenye miaka 29 kutaka kuondoka.

Naelewa kwa Nini Thiago Anaitaka EPL
Thiago

Flick aliiambia Sport1: “Ninaweza kuelewa kuhusu shida ya mchezaji. Thiago alichezea Uhispania kwa FC Barcelona na Bundesliga kwa FC Bayern Munich.”

“Ikiwa anataka kujaribu tena kwenye Ligi Kuu Uingereza kwa sasa, ninamuelewa kabisa. Lakini itakuwa aibu kwa sababu Thiago anaongeza kitu fulani kwenye mchezo wetu.

“Ndiyo maana, kama kocha ningependa ningependa kuwa naye kwenye timu kwa miaka michache ijayo, lakini ndio maisha. Yataendelea.”

Bayern wataumana na Chelsea kwenye mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa ya muzunguko wa mwisho wa mtoano wa timu-16 Jumamosi na baada ya kushinda cha 3-0 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza walipokutana na Stamford Bridge.


Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.

Ingia Mchezoni

36 MAONI

  1. Ameshaona njia imenyooka sasa anaaza madaha nyie kapambaneni ili muwe mbali zaidi mana naona katika mchezo huu mmeshashinda tayari

  2. Thiago anataka baada ya kustaafu awe kumbukumbu ya kucheza Ligi 3 maarufu duniani EPL, BUNDESLIGA na LA LIGA. Namutakia kila la kheri EPL#meridianbettz

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa