Vyanzo vya habari za michezo nchini Italia vinataja kuwa klabu za Napoli na Lazio zinaweza kubadilishana makocha msimu huu wa joto, baada ya Aquile kutajwa kuulizia juu ya upatikanaji wa Gannaro Gattuso.

Mechi dhidi ya Hellas Verona inaonekana kuwa inaweza kuwa mechi ya mwisho ya Gennaro Gattuso akiwa na Napoli, ambaye anatajwa kuwa hayupo tayari kwa suala lolote klabuni hapo zaidi ya kuondoka.

Napoli Kubadilishana Makocha na Lazio
Simone Inzaghi and Gennaro Gattuso
Napoli, 1-08-2020
© Marco Rosi / Fotonotizia

Bado haijawa wazi ni nani ambaye anaweza kuchukua kijiti cha meneja huyu wa zamani wa Milan pale Stadio Diego Maradona, lakini kwa mujibu wa ripoti za Serie A, Luciano Spalletti amekuwa akitajwa tajwa sana na vyanzo mbalimbali.

Kwa upande wa Lazio, wao bado hawajathibitisha ikiwa Inzaghi ataendelea kuwepo kwa msimu wa 2021-22 na vyanzo vinasema kuwa Claudio Lotito ameomba kuonana na Gattuso wiki ijayo.

Kutokana na uhusiano wa klabu hizi mbili, kuna uwezekano mkubwa vilabu vyote vinataka kuangalia namna ya kumaliza suala la wakufunzi, na huenda wakafikia uamuzi wa kubadilishana kama pande zote zitalizia.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Napoli, Napoli Watabadilishana Makocha na Lazio?, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa