Uongozi wa Yanga, unatarajiwa kumpokea kocha ambaye ataifundisha timu hiyo akichukua mikoba ya Mrundi, Cedric Kaze aliyetimuliwa Machi 7, mwaka huu.

Makocha wawili mpaka sasa ndiyo wanatajwa kwamba mmoja wao anaweza kuinoa Yanga ambapo makocha hao wote wamepita Al Merrikh ya Sudan ambao ni Mserbia, Miodrag Ješić na Mtunisia, Nasreddine Nabi.

Yanga Kocha

Ješić ndiye alikuwa wa kwanza kutua Al Merrikh ikiwa ni siku chache tu tangu Didier Gomes kuachana na timu hiyo na kutua Simba alipo sasa.

Siku mbili baada ya Al Merrikh kumtambulisha Ješić kama Mkurugenzi wa Ufundi, ndipo Nasreddine akatambuliwa kuwa kocha mkuu, akaiongoza timu hiyo kwenye mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika akipoteza dhidi ya Al Ahly na AS Vita, kisha sare na Simba, akatimuliwa.

Timu ikakabidhiwa kwa Muingereza, Lee Clark ambaye anainoa timu hiyo kwa sasa ikiwa imeishia hatua ya makundi.

Yanga sqd

Wakati Yanga ikiwa kwenye mchakato wa kumpata mrithi wa Kaze, makocha wengi wamehusishwa akiwemo Nikola Kovazovic, Hubert Velud, Sebastian Migne, kabla ya kuibuka kwa makocha hao wawili.

Tayari Kamati ya Utendaji ya Yanga, imeshampata kocha ambaye atakuja kuinoa timu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.

Baada ya kupitia CV nyingi na kujiridhisha juu ya kocha tunayemuhitaji, Jumapili au Jumatatu, tutakuwa na kazi ya kumpokea kocha wetu mwenye CV kubwa sana Afrika, maana ni kocha aliyewahi kuzinoa moja ya timu kubwa za Sudan.

Tayari tumeshafanya maandalizi yake kwa maana ya kumtumia tiketi na mapokezi, japo ratiba ya ndege ya nchi anayotokea ambayo siwezi kukuambia kwa sasa ilikuwa na mkanganyiko, lakini mambo yamekaa sawa na ndani ya siku mbili hizi nilizokwambia atakuja kujiunga nasi,” kilisema Chanzo hicho.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

yanga, Yanga Kusajili Kocha Mpya, Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa