Kunako muendelezo wa NBA, Milwaukee Bucks wamejinasua kwenye msururu wa vipigo vitatu mfululizo kwenye mchezo dhidi ya LA Lakers.

The Bucks walikuwa uwanjani kuchuana na Lakers usiku wa kuamkia leo ambapo matokeo ya pointi 112-97, yaliwatosha The Bucks kuwaadhibu mabingwa watetezi – Lakers.

Jrue Holiday alipachika pointi 28 akisadiana na Giannis Antetokounmpo ambaye alipachika pointi 25 na kucheza mipira 10 iliyokufa.

Sambamba na kupoteza mchezo huo, mchezaji mpya wa Lakers – Andre Drummond alijikuta akiisaidia timu yake kupata pointi 4 pekee kabla ya kutolewa uwanjani kwa majeruhi ya mguu wake wa kulia.

NBA, NBA: Bucks Wakataa Utumwa mbele ya Lakers., Meridianbet
Andre Drummond akitoka uwanjani baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Milwaukee Bucks.

Lakers walitangaza kuwa vipimo vya awali havijaonesha madhara makubwa kwa Drummond lakini kocha wa timu hiyo – Frank Vogel, amesema Drummond atafanyiwa uchunguzi mwingine mapema Ijumaa hii.

Kitu cha kipekee zaidi kwenye mchezo wa The Bucks vs LA Lakers, ilikuwa ni historia iliyowekwa na ndugu watatu walipokutana kwenye mchezo huu kama wapinzani. Giannis Antetokoumpo akiwa na kaka yake –Thanasis Antetokounmpo ambaye pia wapo timu moja (The Bucks), walikutana uso kwa uso na mwenzao – Kostas Antetokounmpo (Lakers) kwenye mtanange huu.

Kukutana kwa ndugu hawa, kunaweka historia ya kuwa ndugu watatu kukutana kwenye mchezo mmoja wa NBA ikiwa ni mara ya pili kwenye ligi hiyo. Awali ilitokea kwa Aron, Justin na Jrue Holiday mwaka 2019.

Kwingineko kwenye NBA, Brooklyn Nets walishinda kwa matokeo ya pointi 120-108 dhidi ya Houston Rockets. Ushindi wa Nets ulikuwa mchungu kwa James Harden ambaye pia alilazimika kutoka uwanjani baada ya kupata majeruhi.

Phoenix Suns waliwazidi uwezo Chicago Bulls kwa matokeo ya pointi 121-116. Minnesota Timberwolves walitoka nyuma kwa kuzidiwa pointi 13 na kuwashinda New York Knicks kwa pointi 102-101.

Utah Jazz wameendelea kuwa bora msimu huu kwa kuwafunga Memphis Grizzlies kwa pointi 111-107. Miami Heat waliwaadhibu Indiana Pacers kwa pointi 92-87. Dallas Mavericks wameendeleza ubabe kwa kuwapiga Boston Celtics kwa pointi 124-101.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

NBA, NBA: Bucks Wakataa Utumwa mbele ya Lakers., Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa