Wakati ulimwengu wa soka ukiburudika kwa mashindano ya Afcon barani Afrika na World Cup Qualifiers 2022 barani Ulaya, NBA inaendelea kunogesha ulimwengu wa kikapu.

Michezo kadha wa kadha imeendelea wiki hii lakini burudani zaidi ilikuwa pale Brooklyn Nets walipochuana na Detroit Pistons.

Huu ni mchezo ambao Nets walikuwa uwanjani kwa mara ya 31 wakiwa na James Harden msimu huu. Harden alijiunga na Nets akitokea kwenye timu ya Houston Rockets na ameungana na swahiba wake wa muda mrefu , Kevin Durant (KD) ambaye kwa sasa ni majeruhi.

Katika mchezo dhidi ya Pistons, Harden alipachika jumla ya pointi 44 na kutoa pasi 8 za magoli sambamba na kucheza mipira 14 iliyokufa. Mchango wa Harden uliisaidia Nets kuibuka na ushindi wa pointi 113-111.

NBA
Harden (kulia) katika ubora wake dhidi ya Pistons.

Huu ni ushindi wa 26 kati ya michezo 31 ambayo Harden ameitumikia Nets kwenye NBA msimu huu. Baada ya kupachika pointi 44, Harden aligusia kidogo suala la kuwa MVP kwa msimu huu ambapo yeye binafsi anajisikia ni MVP mpaka sasa.

“Ninajihisi kama ninapaswa kuwepo kwenye hayo majadiliano (ya kupewa tuzo ya MVP)? Ninajisikia kama ni MVP.

“Namba zinajionesha na tunashinda michezo yetu. Hilo ndilo ninaloweza kusema. Sitaki kujiongelea sana binafsi yangu. Ninaliacha kama lilivyo.” alisema Harden.

Tuzo ya MVP inatolewa kwa mchezaji aliyefanya vizuri kwenye msimu husika na anapatikana kwa kupigiwa kura na waandishi wa habari wa NBA. Harden aliwahi kupewa tuzo ya MVP mwaka 2018.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

NBA, NBA: Harden Ajipigia Chapuo na uMVP., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa