Wapenzi wa mchezo wa kikapu muda sio mrefu ile hamu ya kuuona msimu mpya wa NBA ukikatwa utepe, itakwisha. Timu mbalimbali kurejea viwanjani na kombe kugombewa upya!!

LA Lakers kufungua duru la msimu mpya wa NBA leo usiku watakapochuana na LA Clippers, huu ni mchezo utakaohitimisha historia ya kuwa na msimu mfupi zaidi wa mashindano hayo kwa msimu wa 2019/20.

NBA, NBA: Msimu Mpya Unakaribia, Hali Ipoje?, Meridianbet
LA Lakers wakiwa na kombe la NBA msimu uliopita.

Sambamba na mchezo wa ufunguzi, Lakers watakabidhiwa medali zao za dhahabu kama ilivyodesturi ya NBA – bingwa wa msimu uliopita anakabidhiwa tuzo hizo mwanzoni mwa msimu unaofuata.

Baadhi ya viwanja vitakuwa na mashabiki wakati ambapo vingine havitokuwa na mashabiki kutokana na taratibu za kujilinda na COVID19.

Tuuangalie msimu mpya wa NBA, yapi yanayojiri msimu huu?

Utawala wa LeBron James Utaendelea?

NBA, NBA: Msimu Mpya Unakaribia, Hali Ipoje?, Meridianbet
LeBron James

James ni ushuhuda wa mtu aliyezaliwa na kipaji chake, ulimwengu wa mchezo wa kikapu unatambua hilo. Akiwa na umri wa miaka 35, bado anatambulika kama mchezaji bora wa muda wote kwenye mchezo huo.

Alipotua LA Lakers 2018, James aliahidi makombe kumfuata na alijitahidi kulitimiza hilo na mwisho wa msimu waliibuka wababe wa NBA msimu uliopita. Sio siri, huwezi kumtaja James bila swahiba wake – Anthony Davis ambaye walikuwa wakishirikiana kufa na kupona kuhakikisha Lakers wamefika walipofika. Vipi msimu huu, James ataendelea kutawala??

Kurejea kwa Kevin Durant au muite ‘Unicorn’.

NBA, NBA: Msimu Mpya Unakaribia, Hali Ipoje?, Meridianbet
Kevin Durant akionesha ubora wake wa kucheza na mpira.

Licha ya kuwa nje ya uwanja kwa sehemu kubwa ya msimu uliopita, Kevin Durant anarejea tena uwanjani msimu huu akiwa na Brooklyn Nets.

Durant anajulikana kwa ufundi wake wa kucheza na mpira na kikapu, uwezo wake wa kupachika magoli kama mshambuliaji ni kati ya vitu vinavyomfanya Durant kuwa mshambuliaji hatari zaidi kwenye NBA.

Upinzani wa Durant vs LeBron James sio wa kitoto. Hawa jamaa wanapokutana uwanjani, mechi hiyo huwa ni ya vuta ni kuvute, ni burudani isiyokifani msimu huu.

Giannis Amelamba Mkataba Mnono Bucks. Je, ataipeperusha vyema bendera ya Bucks?

NBA, NBA: Msimu Mpya Unakaribia, Hali Ipoje?, Meridianbet
Giannis Antetokounmpo katika ubora wakiwa akiwa na Milwaukee Bucks.

Miaka 10 iliyopita, Giannis Antetokounmpo alikuwa akiuza miwani za jua kwenye fukwe za nchi kwako – Ugiriki ili apatefedha ya kuisaidia familia yake. Wiki iliyopita, alisaini mkataba mnono ulioweka historia kwenye Ligi ya NBA baada ya kupata mkataba wa miaka 5 wenye thamani ya dola milioni 228.2

Akiwa na miaka 26 tu, Giannis anashikilia wadhifa wa kuwa MVP na Mlinzi Bora wa Mwaka kwa msimu uliopita. Milwaukee Bucks hawajabeba taji la NBA tangu 1971 na kwa uwekezaji uliofanyika kwa Giannis, ni dhahiri anatarajiwa kulipafadhila kwa kuiongoza timu hiyo kwenye ubingwa msimu huu. Hili litawezekana?

Hakika msimu huu utakuwa wa aina yake. Unadhani timu gani itaibuka kidedea msimu huu?


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

NBA, NBA: Msimu Mpya Unakaribia, Hali Ipoje?, Meridianbet

SOMA ZAIDI

19 MAONI

  1. LA Lakers kufungua duru la msimu mpya wa NBA leo usiku watakapochuana na LA Clippers, huu ni mchezo utakaohitimisha historia ya kuwa na msimu mfupi zaidi wa mashindano hayo kwa msimu wa 2019/20.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa