Mambo yameanza kunoga kuelekea michezo ya Play-Offs kunako ligi ya NBA. Mchezo dhidi ya Toronto Raptors, umewafanya Nets kufuzu hatua ya mtoano mapema zaidi.

Brooklyn Nets walikuwa uwanjani wakichuana na Raptors pale Amalie Arena. Ushindi wa pointi 116-103, unawapa Nets nafasi ya kucheza hatua ya Play-Offs wakitokea katika Eastern Conference.

Kevin Durant na Kyrie Irving walikuwa mihimili ya Nets kwa kupachika pointi 26 katika mchezo ambao wachezaji 7 wa Nets walipachika pointi nyingi kwenye mchezo huo.

“Tumeweka macho yetu kwenye vitu vikubwa, lakini ni hatua nzuri kuwa kwenye nafasi tuliyopo ikiwa imesalia michezo 10.” alisema kocha wa Nets, Steve Nash.

Kwingineko kunako NBA, Giannis Antetokounmpo aliiongoza vyema Milwaukee Bucks kwenye mchezo dhidi ya Charlotte Hornets. Pointi 29 alizopachika Giannis, ziliwatosha Bucks kupata ushindi wa pointi  114-104 na kuendelea kujiimarisha katika nafasi ya 3 kunako msimamo wa Eastern Conference.

Portland Trail Blazers waliwafunga Indiana Pacers kwa pointi 133-112 walipokutana kule Indianapolis.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa