Hakika muda ni suala la kulizingatia katika kuyafikia mafanikio, hakuna kukata tamaa. Phoenix Suns wameondoa ukame uliodumu kwa miaka 11 kunako NBA.

Suns wamefanikiwa kufuzu hatua ya Play-Offs (mtoano) baada ya kuibuka kidedea kwenye mchezo dhidi ya LA Clippers. Mara ya mwisho Suns kufikia hatua hii, ilikuwa msimu wa mwaka 2009-10.

Kwa mara ya kwanza msimu huu, Phoenix Suns wamewafunga LA Clippers na kuendelea kushika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa Western Conference huku Clippers wakishika nafasi ya 3.

NBA, NBA: Phoenix Suns Waiona Nuru Baada ya Miaka 11., Meridianbet
Cris Paul katika ubora wake ndani ya Phoenix Suns.

 

Chris Paul alipachika pointi 28 kati ya 109 zilizowapa ushindi Suns dhidi ya Clippers (pointi 101). Kufuzu kwa Suns kunawaacha Sacramento Kings kwenye kiza cha kuendelea kusota kuifikia hatua ya mtoano kwa miaka 16. Kings wanashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Western Conference kunako NBA msimu huu.

Matokeo mengine kwenye NBA:

Vinara wa Western Conference, Utah Jazz, wameendelea kujiimarisha na kuweka rekodi ya timu yao kwa kuwafunga Sacramento Kings kwa pointi 154-105. Philadelphia 76ers wamefuzu hatua ya mtoano kwa kuwafunga Atlanta Hawks kwa pointi 127-83.

Mabingwa watetezi wa NBA, LA Lakers wanaendelea kutaabika msimu huu baada ya kuambulia kipigo cha pointi 116-107 kutoka kwa Washington Wizards. New York Knicks vs Chicago Bulls (113-94), Boston Celtics vs Charlotte Hornets (120-111), Orlando Magic vs Cleveland Cavaliers (109-104), Denver Nuggets vs New Orleans Pelicans (114-112), Miami Heats vs San Antonio Spurs (116-111) na Portland Trail Blazers vs Memphis Grizzlies (130-109)


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa