Michezo ya Play-in tournament inamalizika leo usiku. Washington Wizards wamefanikiwa kutinga hatua ya Play-Offs kunako NBA msimu huu.

Wizards ambao walipoteza mchezo wao wa kwanza wa play-in dhidi ya Boston Celtics, wanafanikiwa kutinga hatua ya mtoano baada ya kuwaondoa Indiana Pacers kwa pointi 142-115.

Ushindi wa Wizards unawapatia nafasi ya 8 kunako msimamo wa Eastern Conference na sasa watakutana na vinara wa msimamo huo (Philadelphia 76ers) katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano.

Hii ni mara ya kwanza kwa Wizards kufuzu hatua ya mtoano tangu mwaka 2017/18 wakati ikiwa ni mwisho wa safari ya miaka 5 mfululizo kwa Pacers kushiriki hatua ya mtoano.

NBA, NBA: Wizards Wameingia Play-Offs 2021., Meridianbet
Bradley Beal (katikati) alipachika pointi 25 ndani ya dakika 28 alizoitumikia Wizards kwenye mchezo dhidi ya Pacers.

Upande wa pili kwenye NBA, baada ya Golden State Warriors kufungwa na LA Lakers kwenye mchezo wa awali. Warriors sasa watachuana na Memphis Grizzlies ijumaa hii katika mchezo wa kuisaka nafasi ya 8 kunako msimamo wa Western Conference.

Kumalizika kwa michezo ya Regular Season kunako NBA, kunaendana na utoaji wa tuzo kwa wachezaji na makocha waliofanya vizuri kwenye hatua hiyo.

Stephen Curry (Golden State Warriors), Joel Embiid (Philadelphia 76ers) na Nikola Jokic (Denver Nuggets) wanapambania tuzo ya mchezaji bora – Most Valuable Player (MVP).

Quin Snyder (Utah Jazz), Tom Thibodeau (New York Knicks) na Monty Williams (Phoenix Suns), wanapambania tuzo ya kocha bora. Tuzo hizi zitatolewa kabla ya kuanza kwa hatua ya Play-Offs.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

River Plate, River Plate, Enzo Perez Aonesha Uwezo Golini., MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa