Newcastle United wapo kikazi zaidi chini ya utawala mpya. Huko sokoni, wanafanya makubwa. Chris Wood ametua St James’ Park!

Newcastle wamejikuta wakilazimika kusajili mshambuliaji kwenye dirisha hili baada ya Callum Wilson kupata majeruhi ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa muda. Kumkosa Wilson sambamba na hali ilivyo kwenye timu hiyo msimu huu, ni vitu ambavyo uongozi wa klabu hiyo hauwezi kuvivumilia.

Katika kuonesha kwa vitendo kuwa “they mean business”, Newcastle United wamegonga milango kule Turf Moor na sasa, wamevunja mkataba wa Chris Wood na Burnley. Wood alikuwa na kipengele cha dau la £20M kwenye mkataba wake na Burnley.

Newcastle United, Newcastle United Imesajili Chris Wood., Meridianbet
Chris Wood.

Kipengele hiki kimewapa nguvu The Magpies ambao wamelipa pesa hiyo ili kumpata Wood kwenye dirisha hili.

Mchongo umekamilika, Chris Wood sasa ni mchezaji mpya wa Newcastle United baada ya Kieran Trippier.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa