Ni siku 13 toka uongozi mpya wa Newcastle United umeingia madarakani na sasa,  wameamua kumalizana na kocha, Steve Bruce.

Bruce anaondoka Newcastle United baada ya kuiongoza timu hiyo kwa muda wa miaka miwili. Huu ni msimu ambao umekuwa mgumu na mbaya kwa The Magpies, mpaka sasa hawajaonja ladha ya ushindi kwenye EPL ikiwa ni michezo 8 imeshachezwa.

Kuondoka kwa Bruce ni suala ambalo wengi walilitegemea akiwemo Bruce mwenyewe. Kabla ya Mike Ashley kuiuza timu hiyo, Bruce alinukuliwa akisema wazi kuwa, hana uhakika wa kuendelea kuwepo klabuni hapo endapo mabadiliko ya uongozi yatafanyika.

Newcastle United, Newcastle United Yamalizana na Bruce., Meridianbet
Takwimu za Steve Bruce akiwa na Newcastle.

Nukuu ya Steve Bruce, iliendelea kuwa hivyo hata baada ya wamiliki wapya kuingia madarakani na sasa, yametimia!

Baadhi ya makocha wanahusishwa na nafasi ya kukinoa kikosi cha Newcastle United. Kati yao ni Paulo Fonseca, Eddie Howe na Steven Gerrard. Japokuwa Bruce ameachia ngazi, kocha huyu atapewa fidia ya takribani £8M kwa kusitishiwa mkataba wake na klabu hiyo.


KUSANYA MKWANJA NA BIG BAD WOLF

Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa