Alexander Naviatu Vyevye Maandishi "Black Lives Matter" Mechi na Everton.

Trent Alexander-Arnold atavalia viatu vilivyo na maandishi “Black Lives Matter”siku ya mchezo wao dhidi ya Everton lengo ni kuendelea na kusambaza ujumbe unao pinga ubaguzi na kutetea  haki za maisha ya mtu mweusi.

Kufuataia kuuwawa kwa Mmarekani mweusi George Flyod akiwa mikononi mwa polisi mwezi uliyopita yamefanyika  maandamano yanayo lenga kupinga ubaguzi wa rangi ulimwenguni watu mbalimbali mashuhuli wamejaribu kuonesha ujumbe mbalimbali wenye nia ya kutokomeza jambo hilo.

Wachezaji wa mpira katika ligi mbali mbali wamekuwa wa wakivalia tisheti zenye maandishi “Black Lives Matter” juu ya namba zao badala ya Majina, pia wachezaji wamekuwa wakipiga goti chini kwa sekunde tisa kabla mechezo haujaanza.

Manchester City wamethibitisha ya kuwa BLM itaendelea kubaki katika jezi zao mpaka mwisho wa msimu huu.

Liverpool watarudi dimbani kuumana na Everton Jumapili hii na mchezaji wao Alexander-Arnold amepanga kuvaa kiatu chenye ujumbe huo wa “Black  Lives Matter” na kisha kuvifanyia mnada kwa lengo la kukuza mfuko wa fedha katika kituo cha Nelson Mandela.

Trent Alexander-Arnold 

“Tunahitaji kuongea kwa njia nyingine kufikisha ujumbe” aliandika hivyo kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 kwenye mtandao wake wa kijamii “Usiku wa Jumapili kiatu changu kitabeba ujumbe wenye Black Lives Matter.

“Watu weusi wanaonekana tofauti, tuna kabiliana na ubaguzi kwa vitendo ni zaidi ya vurugu na dhulma,fursa za kuishi zimezuiwa katika njia mbalimbali.” Ni ajabu jambo hili kuendelea kuwepo mwaka 2020.

“Mbaya zaidi watu weusi wengi katika jamii zetu wamekuwa wakikumbwa na huu unyanyasaji kila siku, lakini nimatumaini Ulimwengu umeamka kukabiliana na janga hili.”

“Kwa hiyo wakati tuna nafasi, ambapo watu wanaweza kusikiliza, acha tuongee, tuelimishe, tufanye kampeni na acha tuutangaze ujumbe wenye elimu nzuri ili kuleta mabadiliko.

 

52 Komentara

    Huyo ni upendo wa kumthamini mtu mweusi na kuyapinga mauaji ya watu weusi huko Marekani..rest in peas George bado tutamkumbuka

    Jibu

    AAT mkali wa assist pale liverpool.. Dogo anajituma sana. Namkubali sana. #meridianbettz

    Jibu

    Atasaidia pia katika harakati za kutetea mtu mweusi

    Jibu

    Black 👊👊 lives matter PLAY together 🙏🙏🙏

    Jibu

    Kweli kabisa mimi namuunga mkono Alexander kwa kuvaa kiatu hiko na kutokomeza jambo hilo la ubaguzi na kutetea haki za watu weusi 😝😝😝😝😝😝

    Jibu

    Huo Ni mchango katika jamii kuwaamasisha kupinga ubaguzi ila dogo yuko vizuri uwanjani

    Jibu

    Watu weusi wanaonekana tofauti sana na watu wengine hivyo tunapinga ubaguzi wa rangi kwa upande wa michezo imeonekana kuwa mbinu nyingine nikutumia katika michezo ili kuwagikia watu wengi ili kudumisha umoja wa rangi zetu ila leo Everton wanapigwa

    Jibu

    Dogo anajituma Sana mkali wa assist pale liverpool namkubali kinoma

    Jibu

    Watu wengi weusi wamekuwa wakikumbwa na huu hunyanyasaji naimani ulimwengu umeamka kukabiliana na janga hili r i p George flyod

    Jibu

    Ahsant sana meridianbet kwa taarifa

    Jibu

    Huo ndo uzalendo

    Jibu

    Anord beki mahiri wa Liverpool namkubali Sana

    Jibu

    Nimependa iyo

    Jibu

    safi Alexander

    Jibu

    Vizuri Sana kwani kubaguana sio vzr hongera Sana Alexander

    Jibu

    Issue ya George Floyd imekuwa kama njia ya kiberti kuwashwa kwenye msitu mnene. Ndio, moto umewashwa lakini tunahitaji miaka mingi kutokomeza vitendo vya uonevu kwa watu wote duniani sio weusi pekee yao.Maisha ya kila mtu ni muhimu#meridianbettz

    Jibu

    Itakuwa poa.

    Jibu

    Huu ni upendo pia n uthamini wa watu wa jamii yako sehem yoyote ile dunian hongera kwa hilo wenzetu na mataufa makubwa dunian bado wana ile tabia ya kubagua watu weusi

    Jibu

    Nimewapenda bure kwa sababu wanauchungu wa kutetea haki. Hasahasa ubaguzi usiotakiwa

    Jibu

    Ni jambo zuri kupinga ubaguzi wa rangi

    Jibu

    George floyd aliuwawa na wamarekan weupe na walimfanya wawezapo kwa rangi yake sio poa aisee kifo chake wa afrika wote tuliguswa kwa kifo hicho,hivyo bhasi licha ya wachezaji kuvaa jezi za black live matters je watabadilika maana kuvaa sio tatozk ila tatizo kubadilika na kutokombeza ubaguzi wa rang

    Jibu

    Ni vizuri kiendelea kupinga ubaguzi wa rangi

    Jibu

    God bless you Trent ….YNWA

    Jibu

    ITU ni bora sana

    Jibu

    Maoni:Ni kweli inabidi ni kupinga ubaguzi wa rangi.watu weusi wanapata tabu sn wakienda kucheza uko nje

    Jibu

    Safii huo ndo umoja wa watu weusi nimepend hyo

    Jibu

    R.i.p George tutakuenzi daima

    Jibu

    hahahhaah iyo mechi si ya kuikosa kabisa

    Jibu

    Safi Sana mpaka watajua tu kwanini waliwauwa watu weusi

    Jibu

    Ni jambo zuri kuona watu mbalimbali wakijitokeza kupinga vitendo viovu juu ya watu wenye rangi nyeusi duniani

    Jibu

    Ni ubunifu mzur wa kufikisha ujumbe kwa jamii

    Jibu

    Asante meridianbet kwa habari hii

    Jibu

    Watu weusi tumekuwa tofaut kubwa ktk nchi za rangi nyeupe kuendelea kutukandamiza,jamii iliyo Bora itaendelea kupinga ubaguz wa rang duniam kote

    Jibu

    nahisi dunia ishapaza sauti kwa kiwango cha juu sana kama watu hawawezi kubadilisha mitazamo basi badili mtazamo wako hii black lives matter iwe sasa change lives matter

    Jibu

    Niubunifu mzuri sanaa

    Jibu

    Upendo was hali ya juu

    Jibu

    Inaleta faraja kuona watu mbalimbali wanaungana kupinga ubaguzi wa rangi kwa watu weusi

    Jibu

    Ni vizuri kwa kweli#Meridianbettz

    Jibu

    Ni ubunifu mzuri sana

    Jibu

    Itasaidia katika harakati za kusaidia mtu mweus

    Jibu

    Ni vizuri kwake#meridianbettz

    Jibu

    Alitumia njia sahihi kufkisha ujumbe

    Jibu

    Hii n Kali sana maana evarton wakiwa nyuban hawanaga masihala kabisa

    Jibu

    Maisha ya kila mtu ni muhimu#meridianbettz

    Jibu

    Duu jaman nimeipenda hiyo

    Jibu

    Alexander namkubal

    Jibu

    Inapendeza sana kwa Alexander
    # meridianbet

    Jibu

    Nimeipenda kwasababu wanauchungu wakutetea haki haswaa ubaguzi usitakiwa

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Vizuri sana Alexander Mungu akubariki

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Itakuwa vizuri

    Jibu

Acha ujumbe