Alguacil Arefusha Kandarasi Yake na Real Sociedad.

Real Sociedad imemuongeza mkataba mpya Immanol Alguacil utakao fanya kazi mpaka mwaka 2023 baada ya kufanikiwa kuanza msimu vizuri licha ya timu hiyo kupoteza michezo mitatu iliyopita katika LaLiga.

Alguacil Arefusha Kandarasi Yake na Real Sociedad.

Alguacil ameirudisha kilabu kwenye mashindano Europa League wakati wa miaka yake miwili ya uongozi na bodi imeonyesha imani yao kwake kwa kumpa mkataba mpya.

Klabu hiyo pia imeongeza mkataba kwa mkurugenzi wa michezo Roberto Olabe hadi 2024.

Taarifa hiyo inakuja wakati wa kushuka kwa fomu kutoka kwa timu ya Sociedad ambayo haikufungwa katika mechi 10 kwenye mashindano yote kuanzia mwezi Novemba 1 mpaka Desemba 13.

Tangu wakati huo, vijana wa Alguacil wamepata ushindi wa 2-1 huko Barcelona na Levante kabla ya kukubali 2-0 kwa vinara wa LaLiga Atletico Madrid Jumanne.

Baada ya kuwa kocha wa muda mfupi kautoka Machi na Mei 2018, Alguacil alichukua jukumu la Real Sociedad kwa mara ya pili mwezi Desemba 2018, akiisaidia klabu kumaliza nafasi ya tisa katika msimamo wa msimu huo.

Uboreshaji wa mkataba ulifuata 2019-20, wakati Sociedad walimaliza nafasi ya sita na kufanikiwa kufuzu katika Ligi ya Europa, ambapo walimaliza wa pili kwenye Kundi F nyuma ya Napoli.

Rais wa klabu Jokin Aperribay alizungumzia fahari yake kwa mafanikio ya klabu hivi karibuni, akiongea kwenye mkutano mkuu wa wanahisa: “Tunakabiliwa na miaka miwili ya kutokuwa na uhakika mkubwa. Janga hili limetuathiri katika misimu ya 2019-20 na 2020-21.

“Tunajivunia kuweza kutoa matokeo mazuri licha ya nyakati tunazopitia.”


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

14 Komentara

    Yuko sahihi

    Jibu

    Ukiwaangalia Real Sociedad wamebadilika sana huenda Alguacil akaibadilisha zaidi nahisi anahitaji muda kidogo tuu kudhihirisha ubora wake

    Jibu

    Ni kweli kabisah

    Jibu

    Yupo sahihi

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Yuko saihii

    Jibu

    Duhh atarii

    Jibu

    Yopo sahii

    Jibu

    Anajua ninkinatakiw

    Jibu

    Not bad

    Jibu

    Yupo sahihi

    Jibu

    Yuko sahihi

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Kajitahidi Sana kwakweli

    Jibu

Acha ujumbe