Anthony Martial Yuko Wapi? Ni Sintofahamu Ndani ya Man United

Wakati maandalizi ya msimu mpya wa EPL yakiendelea pale Carrington, Manchester. Anthony Martial bado haonekani kwenye kamera za waandishi. Kulikoni?

Martial alipata majeraha ya goti akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa mwezi Aprili,2021. Kuumia kule kulimuweka nje ya uwanja kwa muda wote wa msimu wa 2020/21 uliokua umebakia.

Japokuwa taarifa kutoka Ufaransa ziliripoti kuwa majeraha ya Anthony Martial hayakuwa makubwa, mambo yalikua tofauti baada ya kufanyiwa vipimo alivyorejea United. Ole Gunnar Solskjaer aliondoa matumaini ya kumtumia Martial kwenye fainali ya Europa kutokana na taarifa ya madaktari kuhusu hali ya mchezaji huyo.

Siku zikaenda, United wakaendelea na maisha bila Anthony Martial. 2021/22 hii hapa. Martial hajarejea United mpaka sasa na hakuna taarifa kamili inayozungumzia hali yake au pengine wapi alipo?

Rashford akiwa na Sancho

United wamemsajili Jadon Sancho na sasa idara ya ushambuliaji inaubora na upana wa kumtosha Ole kufanya maajabu yake uwanjani. Bado haijajulikana kama Sancho atapewa jezi namba 7 au la? Endapo itatokea hivo, Edinson Cavani anauwezekano mkubwa wa kupewa jezi namba 9 ambayo imekuwa ikitumiwa na Martial tangu ajiunge United (2015).

2020/21 ulikua n msimu mbaya zaidi kwa Anthony Martial tangu atue United. Alizifumania nyavu mara 7 pekee huku akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara. Uwepo wa Cavani na Greenwood uliiokoa United kutokana na washambuliaji hao kuwa na kiwango bora kwenye kuzifumania nyavu za mashabiki. Martial utacheza namba ya nani kwa sasa? 

Wakati tukisubiria muda ufike kwa Marcus Rashford kufanyiwa upasuaji wa bega ambao utamuweka nje ya uwanja mpaka mwezi Oktoba, bado Martial haonekani uwanjani na hii inatoa nafasi kwa Dan James, Juan Mata, Sancho na Greenwood kuonesha ubora wao wakati Rashford akiuguza jeraha lake na pengine Martial akiwa anafanya hivyo tangu April,2021.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe