Antonio Conte Kuhusu Spurs.

London: Kocha wa timu ya Tottenham Spurs Antonio Conte amefanya mahojiano na Skysports na ameongea mengi kuhusu timu yake kupata ukomavu mzuri kukabiliana na mechi tofauti.

Spurs hii leo atakuwa mgeni wa Nottingham Forest katika mchezo wake wa nne ambapo mpaka sasa amejikusanyia alama saba kwenye michezo mitatu ambayo amekwisha cheza mpaka sasa. Amepata ushindi mara mbili na sare moja, wakati huo kwa upande wa Nottingham Forest mpaka sasa wapo kwenye nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi huku wakiwa wamecheza michezo mitatu na wakiwa na alama 4.Antonio Conte

Antonio Conte amesema kuwa ana furaha kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya. Lakini pia aliongezea kwa kusema aliposajiliwa kuwa kama kocha mkuu wa Spurs mwezi November hakuna mtu aliyetarajia kama wangeweza kushriki michuano hiyo mikubwa Ulaya kwasababu timu ilikuwa na wakati mgumu sana.

Hatukuanza kutoka mwanzo, tulianza katika kiwango cha kati na sasa tunaendelea kuboresha kipengele chetu cha mbinu kwa kutekeleza mawazo mapya”

Antonio Conte kuhusu Spurs

Lakini pia aliongelea maingizo ya wachezaji wapya ambao wamewasajili msimu huu kama kina Richalson, Yves Bissouma, Ivan Perisich, na Djed Spence, kuondoka kwa Ndombele, Lo Celso, na Steve Bergwijn na wengine wengi kumeboresha kikosi chao ambapo kipo chini ya Antonio Conte.

Acha ujumbe