Klabu ya Aston Villa imekamilisha usajiri wa mlinzi wa klabu ya Sevilla Diego Carlos kwa ada ambayo pande zote mbili hawakutaka kuweka wazi ni kiasi gani kimetumika kukamilisha  usajiri wa mlinzi huyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazili mwenye umri wa miaka 29 amewasili kwenye dimba la Villa Park na kuweka wino wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka minne baada ya kukamilisha vipimo vya afya na kukubaliana masharti binafsi.

Aston Villa, Aston Villa Wakamilisha Usajiri wa Diego Carlos, Meridianbet

Kocha wa klabu ya Aston Villa Steven Gerrard amekuwa akiimarisha kikosi chake kwa ajiri ya msimu ujao, na mpaka sasa tayari kashakamilisha sajiri ya Philippe Coutinho na Boubacar Kamara.

Diego Carlos alinukuliwa na mtandao wa klabu: “Kiukweli nina furaha kwa sababu ligi kuu ya Uingereza ni moja ya ligi yenye ushindani bora.

“Na mara zote nataka kufanya vizuri kwa klabu na jersey ninayoivaa. hata sasa siwezi kuamini nipo hapa kukamilisha ndoto za ligi kuu ya Uingereza.

“Na sasa nina nafasi nyeupe, natumaini nitajitoa kwa asilimia 100, na kuweza kucheza kwa ubora na uwezo wangu wote.”


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa