Klabu ya Atalanta wamepanga kumsajili moja kwa moja beki wa Juventus Merih Demiral ambaye wapo naye klabuni hapo kwa mkopo.

Demiral alitua Atalanta kwa dili ya mkopo akitokea Bianconeri majira ya joto mwaka jana huku kukikwa na kipengele cha kumnunua kwa dau la €28m,  na alikuwa mchezaji muhimu kwa Atalanta msimu huu uliyomalizika wikendi iliyopita baada ya kuonyesha kiwango thabiti.

Kwa mujibu wa mwandishi Fabrizio ni kwamba Atalanta wanataka kuamilisha uhamisho wa kudumu wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki haraka iwezekanavyo licha ya timu hiyo kutoshiriki michuano ya Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza ligi katika nafasi ya nane.

Ikumbukwe La Dea na Bianconeri wanauhusiano mzuri kwenye kuuziana wachezaji  na Demiral aliondoka Juve kwa sababu hakuwa akicheza mechi za kutosha, na hata alituma ujumbe wa kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo.

Timu ya sasa ya Juve ni nzuri vya kutosha, si rahisi tena kwa Demiral kupatana nafasi tena  ya kucheza hivyo Demiral kuwekwa sokoni ni kitu kisicho epukika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa