UONGOZI wa Azam umetamba kuwa usajili mkubwa ambao wanaufanya kuelekea msimu ujao unaonyesha wazi kuwa kuna kitu wamedhamiria kukifanya hususani katika mashindano ya kimataifa.

Azam mpaka sasa wamekamilisha usajili na kuwatangaza mastaa watano wapya ambao ni viungo, Issa Ndala, Abdul Sopu, Cleophas Mkandala, Tape Edinho na mshambuliaji, Kipre Junior huku wakiachana na kipa, Mathias Kigonya na kiungo Frank Domayo.

Azam inatarajiwa kuwa mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, kufuatia kumaliza kwenye nafasi ya tatu kwnye msimamo wa msimu uliopita wa ligi baada ya kukusanya pointi 49 katika michezo yao 30 waliyocheza.

Mkuu wa Idara  ya Habari na Mawasiliano wa Azam, Thabith Zakaria ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Tupo kwenye taratibu za maboresho ya kikosi chetu, kama ambavyo mnaona tunaendelea kutangaza wachezaji wapya ambao wanakuja kuongeza nguvu ndani ya kikosi chetu kuelekea msimu ujao.

“Nguvu hii kubwa ambayo inaonekana kwetu ina maana kuwa tumedhamiria kufanya jambo la tofauti msimu ujao, tuna nafasi ya ushiriki kimataifa na tunataka kuhakikisha tunafanya vizuri katika michuano hiyo na ile ya ndani.”

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa