Klabu ya Azam FC imemtangaza  kocha mpya ambaye anatarajia kukisuka kikosi hicho kwa msimu huu mpya wa 2022/2023. Kocha huyo ambaye ni raia wa Ufaransa anajulikana kwa jina la Denis Lavagne.

Azam Yashusha Kocha Mpya

Kocha huyo amewahi kufundisha  timu ya taifa ya Cameroon, timu mbalimbali za Afrika ikiwemo Camerron, Algeria, Misri na Tunisia ambapo kocha huyo ana leseni kubwa ya Uefa Pro na leo hii atakuwa jukwaani kutazama Azam wakivaana na Yanga.

Timu hiyo ambayo siku si nyingi imemfukuza kocha aliyekuwa kocha wao Abdihamid Moallin kutokana na timu hiyo kutoridhishwa na kiwango chake na presha iliongezeka zaidi baada ya kutoa sare mchezo wao wa ligi ambao walicheza dhidi ya Geita Gold na kupata sare ya 1-1.

Azam Yashusha Kocha Mpya

Azam Fc ambao wanashiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Africa walikuwa wanahitaji kumtangaza kocha mpya mapema ili aweze kujuana na wachezaji kwani michuano hiyo imebaki siku chache ianze.

Matajiri hao wa Chamazi wamefanya sajili za wachezaji mbalimbali ili kuja kupigania ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara lakini pia na kufanya vyema kwenye michuano hiyo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa