Thomas Tuchel ametimuliwa Chelsea kufuatia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Dinamo Zagreb kwenye Ligi ya Mabingwa.

Mmiliki mpya wa Chelsea, Todd Boehly hajapoteza muda kumfungia kocha huyo wa Ujerumani akiwa na mechi saba pekee msimu huu, siku 100 tangu achukue nafasi ya Roman Abramovich.

Baada ya Tuchel kutimuliwa Chelsea, Kocha Mpya Ajaye Huyu Hapa

Chelsea wako katika nafasi ya sita kwenye Ligi ya Epl na wameanza vibaya kampeni zao za Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Tuchel akiwa amepoteza nafasi yake saa chache baada ya kupoteza kwa bao 1-0 huko Croatia, ikiwa ni mechi yake ya 100 kuongoza.

Katika taarifa hiyo Chelsea iliandika: “Kwa niaba ya kila mtu katika Chelsea FC, klabu ingependa kuweka rekodi ya shukurani zake kwa Thomas na wafanyakazi wake kwa juhudi zao zote wakati wakiwa na Klabu. Thomas atakuwa na nafasi katika historia ya Chelsea baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa, Kombe la Super Cup na Kombe la Dunia la vilabu katika wakati wake hapa”.

Baada ya Tuchel kutimuliwa Chelsea, Kocha Mpya Ajaye Huyu Hapa

Wakati wamiliki hao wapya wa Chelsea kufikisha siku 100 tangu kuchukua Klabu hiyo, na huku wakiendelea na kazi yake kubwa ya kuipeleka klabu mbele, wamiliki wapya wanaamini kuwa ni wakati mwafaka wa kufanya mabadiliko haya.’

Kwa mujibu wa Sportsmail inaelewa kuwa, bosi wa Brighton Graham Potter ni kama mshindani anayeongoza mapema kuwania nafasi ya kuinoa Chelsea, wakati Mauricio Pochettino ambaye hana kazi pia anazingatiwa.

Baada ya Tuchel kutimuliwa Chelsea, Kocha Mpya Ajaye Huyu Hapa
Graham Potter

Chelsea iliongeza kuwa watafanya ‘haraka’ kuteua meneja mpya na wakufunzi wa Tuchel watachukua jukumu la kuinoa timu kwa muda.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa