Muda wa Gareth Bale na Real Madrid umefika mwisho ambapo mkataba wake utaacha kufanya kazi Juni 30 na tayari amewaaga Real Madrid.

Kwa miaka mingi Bale am,ekuwa akihusishwa kutemana na klabu hiyo ya Laliga na mwaka 2019 iliripotiwa yupo njiani kujiunga na ligi ya China lakini badala yake alijiungs na Tottenhma kwa mkopo na baadaye kurejea Bernabeu.

Sasa, baada ya kuaga katika uwanja wa Santiago Bernabeu, kuna tetesi kuhusu uwezekano wake wa kustaafu soka.

Hata hivyo, Bale, 32, hataki kuzungumzia uvumi, akisisitiza kwamba uamuzi wake hautategemea kama Wales itafuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

“Sio lazima, hapana,” Bale alisema, aliulizwa kama kufuzu kwa Wales kunaweza kuathiri uamuzi wake, iliyoripotiwa na Mirror. “Kama nilivyosema hapo awali, siangazii hayo.

“Tuna mchezo muhimu sana. Sihitaji kufikiria au kuwa na wasiwasi kuhusu kitu kingine chochote.”


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa