Buffon Kurejea Nyumbani, Parma.

Inaripotiwa kuwa, aliyekuwa golikipa wa Juventus – Gigi Buffon yupo mbioni kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Parma.

Licha ya kwamba Parma haichezi ligi ya Serie A, Buffon anahistoria na klabu hii ambapo ndipo alipoanzia maisha yake ya soka mnamo mwaka 1995 kabla ya kujiunga na Juventus mwaka 2001.

Alipokuwa Parma wakati huo, alifanikiwa kubeba mataji matatu –Uefa Cup, Italian Cup na Italian Super Cup yote ya mwaka 1999. Aliitumikia Parma kwa jumla ya michezo 220.

Baada ya kujinga na Juventus, Buffon aliitumikia klabu hiyo kwa misimu 19 ikiwa ni pamoja na kucheza jumla ya michezo 685. Licha ya kuwa na umri wa miaka 43 kwa sasa, Gigi alipokea mapendekezo ya usajili kutoka Besiktas na Barcelona lakini ripoti zinasema ameamua kurudi nyumbani, Parma.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

3 Komentara

    Kama karejea safi

    Jibu

    Amefanya kazi kubwa sana katika ulimwengu wa Soka, Heshima kwake

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe