Jamie Carragher beki wa zamani wa Liverpool amezungumza kuhusiana na kufukuzwa kazi kwa aliekua kocha wa timu hiyo Thomas Tuchel.

Carragher anaeleza haamini kama bosi mpya wa timu hiyo bwana Tody Boehly angekua katili kwa kiwango hicho kwakua aliamini baada ya utawala wa bilionea wa kirusi Roman Abramovic kupita basi Chelsea wangeachana na utaratibu wa kufukuza makocha mara kwa mara lakini hali imekua tofauti.

jamie carragherCarragher anaamini ingekua utawala wa Abramovic basi angemuhofia Tuchel kwa matokeo yanayoendelea kwani ilionekana kwa makocha kadhaa waliopita na waliofanikiwa kwa timu hiyo kama Jose Mourinho,Carlo Anchelotti,pamoja Antonio Conte lakini walitimuliwa pale tu timu ilipoanza kufanya vibaya bila kuangalia mafanikio yao.

Carragher pia ameongeza kwa kusema ana wasiwasi mkubwa na kocha anayehusishwa zaidi kuchukua nafasi ya Tuchel kocha wa Brighton mwingereza Graham Potter kua timu ya Chelsea haiamini sana kwenye maendeleo ya muda mrefu jambo ambalo linaweza likamgharimu kocha huyto raia wa Uingereza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa