Chelsea the blues mabingwa wa zamani wa ulaya metaarifiwa wamemalizana na kocha wa Brighton and Hove Albion Graham Potter mapema leo hii.

Klabu hiyo ambayo kwasasa haina kocha mkuu baada ya kumtimua kocha wake mkuu jana mjerumani Thomas Tuchel baada ya mfululizo wa matokeo mabaya klabuni hapo tangu kuanza kwa msimu huu na timu kubakizwa mikononi mwa waliokua wasaidizi wa kocha.

chelseaChelsea wamefikia makubaliano na kocha huyo raia wa Uingereza kukinoa kikosi hicho na kilichobakia ni kutangazwa rasmi kocha huyo atakaechukua mikoba ya Thomas Tuchel.

Kocha huyo ambae amefanikiwa kuitengeneza timu ya Brighton kua timu tishio za kati kwenye ligi kuu Uingereza akiwa muumini wa soka safi na la kushambulia.

Imetaarifiwa mapema leo asubuhi kocha huyo alifika kwenye viunga vya Brighton kwajili ya kuwaaga timu yake hiyo na kuanza safari rasmi ya kuelekea darajani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa