Ed Woodward ameonya haitokuwa biashara kama kawaida kwa United kwenye dirisha la usajili kipindi cha kiangazi, na taarifa zinazosambaa kuwa klabu inahusishwa kusajili wachezaji kwa pauni milioni mia ” mbali na ukweli”
Ole Gunnar Solskjaer ana matumanini ya saini za wachezaji wapya kwenye kikosi chake pale dirisha likifunguliwa na labu inaendelea kufuatilia wachezaji wanahitajika, lakini kutoka na matokeo ya COVID-19 inaweza kupelekea kupunguza matumizi katika soko.
Winga wa Dortmund, Jadon Sancho ndio kinara kwenye orodha na Harry Kane pia anawindwa na United ili kuziba pengo la Romelu Lukaku, ambaye alihamia Inter msimu uliopita. Lakini mazungumzo na nahodha wa Uingereza, Kane kwa usajili £200 million yamesitishwa.
“Wote tupo katika mawazo kuhusu changamoto inayokumba mpira wa miguu kwasasa na katika usajili haitokuwa biashara kama tulivyozoea kwa vilabu, tukiwemo sisi kwenye soko la usajili kipindi hiki cha majira ya kiangazi”. Ed Woodward amesema kwenye forum ya mashabiki Ijumaa.
“Siku zote kipaumbele ni mafanikio katika timu, lakini kwasasa kutoka na janga la Corona biashara ya mpira wa miguu imeadhirika, ikiwemo muda wa kufanya usajili lakini pia kiuchumu, kabla hatujaongelea kurejea kwenye hali ya kawaida.
“Kwa hali hii, siwezi kujisikia vizuri kuzungumzia usajili wa pauni milioni mia wa mchezaji mmoja kipindi cha kiangazi inamaana, hufuatilii changamoto zinzokupa michezo.”
Kwasasa Ligi kuu imesimishwa kutokana na janga la Corona na hakuna tarehe rasmi ya kumalizia msimu.
Issa
Inabidi atumie pesa nyingi tu kufanya usajili