Edwin Van der sar ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu ya Ajax mpaka 2025 kana afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 51 amekua kwenye bodi ya timu hiyo kwa muongo mmoja sasa lakini alikabidhiwa majukumu aliyokua nayo hivi sasa rasmi klabuni hapo mwaka 2016 katika mkataba wa gwiji huyo ulikua unamalizika mwaka 2023 lakini ameongeza miaka mingine miwili hivo atasalia klabuni hapo mpaka mwaka 2025.

edwin van der sarNyota huyo wa zamani wa vilabu vya Ajax,Juventus,Fulham na Man united amekua chachu ya kuendeleza utamaduni wa klabu hiyo yenye historia ya kutengeneza vipaji bora na soka la kuvutia barani ulaya.

Edwin akiongea alisema lengo kubwa zaidi ni kua sehemu ya muundo wa timu bora ya kimataifa pia anaeleza kuanzia mwaka 2024 kutakua na mfumo wa ligi ya mabingwa ulaya na kusisitiza wanahitaji kushindana kila mwaka katika mfumo mpya wa ligi ya mabingwa ulaya.

Edwin anasema safari hiyo haina mwisho anahitaji kuendelea kutoa mchango wake katika mchakato huo anashirikiana kila siku na wenzake sio tun kuipambania timu ya kwanza bali kuhakikisha timu za vijana na wanawake zinafanya vizuri.

Katika utawala wa Van der sar Ajax wamefanikiwa kushinda mataji matano katika miaka sita ya utawala wake likiwemo taji la ligi kuu ya Uholanzi maarufu kama Eredivise katika misimu mitatu kati ya minne iliyopita.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa