Aliyekuwa kocha wa magolikipa wa Manchester United, Emilio Alvarez amesema kuwa golikipa David de Gea ndiye alikuwa sababu ya yeye kuondoka klabuni hapo.

Alvarez alimfundisha golikipa huyu alipokuwa Atletico Madrid, lakini pia alipata nafasi ya kufanya naye kazi pale Manchester United, kabla hajaamua kuondoka Old Trafford Septemba mwaka jana.

Alvarez anasema kuwa alimsaidia golikipa De Gea mwaka 2011. Lakini ansema aliondoka United kwa sababu hakuwa anataka tena kuendelea kumfundisha De Gea.

Kulikuwa na tetesi kuwa klabu iliamua kumsimamisha majukumu yake. Laini, kwa mujibu wa mkufunzi, anakanusha kuwa si kweli kuwa Manchester United walimfuta kazi. Bali aliamua kuondoka klabuni hapo.

Emilio Alvarez: De Gea Alifanya Niondoke United
De Gea na Alvarez walikuwa karibu

“Ilikuwa ni kwenye kikao fulani. Walikuwa wanataka niongeze mkataba, nikawaambia kuwa siwezi kuongeza kwa kuwa sitaki kuendelea kumfundisha De Gea.”

Ukiacha kuwa mshauri wake mzuri kule Atletico Madrid, ambako Emilio Alvarez alimsaidia kuwa moja ya makipa bora zaidi. Alvarez anasema yeye ndiye alimshawishi golikipa huyu kusaini mkataba na klabu ya Man United.

Kocha huyu wa zamani anamlaumu De Gea kwa kusaini mkataba wake unaomuweka Man U hadi 2023 bila yeye kufahamu. Kitu ambacho anakiona kama ni kukosa uaminifu kutokana na uhusiano waliokuwa nao.


Kuna ofa kibao sana unazofaidi ikiwa unabashiri na Meridianbet. Jiunge sasa kufurahia ofa zetu

Bonyeza HAPA Kujiunga.

49 MAONI

  1. Du Emilio Alvarez ameniacha mdomo wazi bila shaka kuna mahali alitaka De Gea aende mwisho ameona lengo lake halijatimia ameamua kufungasha virago#meridianbettz

  2. Ukiacha kuwa mshauri wake mzuri kule Atletico Madrid, ambako Emilio Alvarez alimsaidia kuwa moja ya makipa bora zaidi. Alvarez anasema yeye ndiye alimshawishi golikipa huyu kusaini mkataba na klabu ya Man United.

  3. Mmmh hapa kunakitu kwanini Emilio amlaumu De Gea kusaini mkataba unaomuweka man u na kukataa tuhuma zinazomkabili za yeye kufukuzwa man u hizi tuhuma zinaweza kua za kweli kuna kitu walikiona uongozi wa Manchester united ndio maana wakamtimua Emilio Alvarez pengine alitaka kumuondoa De Gea man u

  4. De gea ni goli kipa mzuri sana pia alves sijui kwa nini anaonekana kama ajapendezewa na kipa huyo na kusema alikuwa ataki kuendelea kumfundisha tena de gea

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa