Epl kusimama mwishoni mwa wiki hii kufuatia kifo cha malkia Elizabeth kilichotokea mapema jana huko kwenye jumba la kifalme linalofahamika kama Balmoral.

Taarifa ya kusimama kwa ligi kuu ya Uingereza imetoka mapema leo mchana kwajili ya kupisha maombolezo ya kifo cha malkia Elizabeth kilichotokea jana.

eplBaada ya taarifa ya kifo hicho kutokea kulikua na michuano ya Europe League ambayo pia ilionesha ishara ya kuomboleza kifo cha malkia michezo ilikua kama Man united iliyokua nyumbani dhidi ya Real sociedad,West ham united pia walikua nyumbani dhidi ya Fc FCSB na michezo mingine yote iliyochezwa jana walisimama dakika chache kabla ya mchezo kuomboleza kifo cha malkia kilichotokea jana.

Kuna michezo kadhaa ambayo ingeendelea mwishoni mwa wiki hii basi michezo hiyo haitaendelea kesho jumamosi na jumapili kutokana kilichotokea nchini Uingereza mpaka wakati mwingine tena.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa