EPL: Wachezaji Wagoma Kukatwa 30%

Wachezaji wa Ligi kuu England (EPL), wamegoma kukatwa mishahara yao katika kipindi hiki, licha ya kuelezwa kwamba klabu zao zitapata hasara ya pauni bilioni 1.137 kutokana janga la virusi vya Corona.

Mkutano wa video uliofanyika leo mchana, ambapo klabu zimewakilishwa na Manahodha na makocha wao, wamezitaka klabu kuwaeleza sababu madhubuti za kwanini wakubali kukatwa mishahara

Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne, Nahodha wa Watford, Troy Deeney na West Ham, Mark Noble walionekana kipinga hilo katika mkutano huo wa video, uliofanyika Jumamosi saa tisa ukihudhuriwa na mwakilishi wa wachezaji kutoka kila timu, kocha na watendaji wakuu wa vilabu.

Kevin De Bruyne na Mo Salah

Moja wa wachezaji alisema “Ni bora pesa yetu tuwape NHS kuliko kuwasaidia matajiri wamiliki.

Waliambiwa kuwa kwa hali ya sasa kama msimu wa 2019/2020 hautaendelea gharama za klabu zitafika £1billion kwani tutakuwa tumepoteza haki za matangazo, mapato ya mechi na mapato ya mdhamini.

Mambo yalibaki kuwa magumu kwani mkutano huo iliisha bila kupata muafaka, hivyo klabu zimewataka wachezaji kufikiria upya juu ya jambo hilo.

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Bora wakae chini wafikie makubaliano

    Jibu

Acha ujumbe