KIUNGO mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amekiri kuwa bao alilofunga leo Jumatano, Februari 23, 2022 dhidi ya Mtibwa Sugar alifunga kwa mkono badala ya kichwa kama ambavyo ilidhaniwa katika mchezo huo wa NBC Premier League kwenye Dimba la Manungu Tuliani.

Fei Toto alifunga bao hilo kunako dakika ya 46 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Said Ntibazonkiza ‘Saido’ ambapo Feisal alionekana kama ameruka na kupiga kichwa na kuzamisha wavuni kumbe mpira ule aliudhamisha wavuni kwa mkono na kuanza kushangilia.

Fei toto
Fei toto

Hata hivyo, mwamuzi wa mchezo huo, Joachim Akamba kutoka Mbeya alilikataa bao hilo na kumpiga kadi ya njano fundi huyo wa soka kutoka Zenji.

Akihojiwa na Azam TV baada kumalizika kwa mchezo huo, Feisal amekiri kufunga bao hilo kwa mkono; “Inatokea katika mchezo, si unajua mambo kama hayo huwa yanatokea….” alisema Feisal.

Akizungumzia mwendelezo wa ushindi wa timu yake, Feisal amesema lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanashinda Ubingwa wa Ligi Kuu mwaka huu, hivyo watahakikisha wanapambana kufa na kupona kila mechi ili kuwapa furaha mashabiki wao msimu huu kwa kushinda kombe hilo.

Hata hivyo mechi hiyo imemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Mtibwa, mabao yakifungwa Said Ntibazoinkiza dakika ya 45+6 na Fiston Mayeye dakika ya 67 na kuifanya Yanga kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu wakiwa na pointi 39 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 31.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa