Kiungo wa Manchester City Phil Foden ameibuka mchezaji bora chipukizi wa msimu kwa mara ya pili mfululizo katika tuzo zilizotolewa na Premier League kwa kuwapiku Declan Rice, Mason Mount, Saka na wengine.
Kinda huyo wa miaka 21 amefunga mabao 9 na kusaidia mengine matano katika michezo 27 ya ligi na kuisaidia City kuwa katika nafasi ya kutetea taji la Premier League ambapo City wanajiandaa kukabiliana na Aston Villa siku ya Jumapili mchezo wa kuamua ubingwa.
“Najisikia furaha kushinda tuzo hii kwa mara ya pili mfululizo kuna wachezaji wengi wenye vipaji kwenye Premkier League na ni heshima kubwa kushinda tena.” alisema Foden
Foden ameshinda tuzo hiyo kwa kura zilizopigwa na mashabiki pamoja jopo la Premier League.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.