Griezmann Apata Jeraha Kubwa.

Mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann amepata majeraha kwenye misuli ya paja, Klabu hiyo ya LaLiga imethibitisha.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitolewa na nafasi yake ilichukuliwa na Luis Suarez kwenye mchezo dhidi ya Real Valladolid ambapo Barcelona walishinda 1-0  ugenini siku ya Jumamosi.

Baada ya vipimo siku yaJumapili vinaonesha Griezmann alipata mvunjiko karibia na goti katika mguu wake wa kulia na itapelekea kukaa nje ya dimba kwa muda.

Mshindi huyo wa kombe la Dunia mwaka 2018, alihamia katika timu ya Barcelona akitokea Atletico Madrid kwa kitita cha €120m mwaka uliyopita. Griezmann ni kama ataukosa mchezo dhidi ys Osasuna siku ya Alhamisi utakao pigwa katika dimba la Camp Nou.

Griezmann amefunga goli tisa katika michezo 35 ya ligi akiwa na Barcelona katika msimu wake mgumu wa kwanza.

Hakujumuishwa katika kikosi cha kwanza kwenye michezo miwili ambayo Barcelona walipata matokeo ya sare ya 2-2 dhidi ya Celta Vigo na Atletico Madrid mwezi uliyopita, lakini alihusika kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Villarreal baada ya kuwekwa kwenye kikosi cha kwanza siku ya Julai 5.


51 Komentara

    Ni mchezaji mzuri sema toka ajiunge na Barcelona ajaendana na fomesheni yake

    Jibu

    Antonio Griezmann hana bahati na Barcelona.Kiwango chake sio cha kuridhisha sana#meridianbettz

    Jibu

    Pole sana kijana huu ndio ulikuwa mda wa kuonyesha uwezo wako sasa umepata jeraha inabidi upumzike

    Jibu

    Get well soon griezmann

    Jibu

    Pole sana kijana utapa nafuu

    Jibu

    Pole yake
    Popote ulipo

    Jibu

    Utapata nafuu utapona

    Jibu

    Duu pole yako Griezmann

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Pole sana kwake japo barca ina wachezaji wengi ambao wataziba pengo lake

    Jibu

    Pole sana grizmann kwa kupata ajali kwenye misuli ya paja utapona na mambo mengine yataendelea

    Jibu

    Ugua pole champ

    Jibu

    Pole yake#Meridianbettz

    Jibu

    Hill ni tatizo kwa Barcelona

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Pole griezmann ila Barca Ina watu wengi wenye uwezo wa kukava iyo nafasi

    Jibu

    Pole griezman

    Jibu

    Duh pole Sana Antonio grezman litakuwa pengo kubwa Sana kwa Barcelona

    Jibu

    So sad story kwa washabiki wa Bac

    Jibu

    pole sana

    Jibu

    Pole yake#meridianbettz

    Jibu

    Pole Sana ucijali utapata nafuu

    Jibu

    Kuumia kwa Griezmann ni balaa sana kwa Barca

    Jibu

    Kipnd ichi team inamuitaji san

    Jibu

    Pole Sana kuumia kwake ni pigo Barcelona

    Jibu

    daah! pole sana ni habari mbaya kwa Barcelona kuelekea kutwaa ubingwa wa laliga msimu huu

    Jibu

    Ni habari mbaya sana kwa timu sema ni mchezaji ambaye ana bahati mbaya sana kwa timu

    Jibu

    Ndo mpira hulivyo utapona tu.

    Jibu

    Matokeo ya mpira hayo yeye kapata jeraha sawa kuna wengne wanakufa uwanjani ila kwa kuumia kwake itafanya barca kisuasua kukimbizana na real madrid kwenye mbio za ubingwa wa laliga

    Jibu

    Mpira hauna mjuaji

    Jibu

    Habari ya kusikitisha. Pole kwa majeraha Griezmann

    Jibu

    Ni pengo kwa Barcelona.

    Jibu

    Habari mbaya kwa club ya backa

    Jibu

    Pole yakee

    Jibu

    Pengo kubwa kwa Barcelona

    Jibu

    Pole San pengo kubwa kwa baca ucjl utapata nafuu

    Jibu

    Pole sana Griezmann

    Jibu

    Daah! Ni balaa ilo kwa Barcelona hasa kipindi iki cha kuelekea kwenye ubingwa

    Jibu

    Yani baada ya kujiunga na Barcelona Kama amekuwa na fundi kiwango kimeshuka na angepoteza ubora wake kabisaa

    Jibu

    Pole sana kijana

    Jibu

    huyu kaenda na mkosi aisee hapati n number akipata ndo hivi aisee

    Jibu

    Jamani pole yake Griezmann

    Jibu

    Pole Sana, mungu atakufanyia wepesi utapona

    Jibu

    Inshallah atapona

    Jibu

    Huyu siku hizi anaumia sana#Meridianbettz

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Habari mbaya kwa clabu zima ya Barcelona na mashabiki wake kwa hujumla

    Jibu

    Grizman kuumia kwake kunaleta presha kubwa kwa shabiki wa Barcelona

    Jibu

    Habar ya kusikitisha sana

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Maoni:pole sana

    Jibu

Acha ujumbe