Rashford alipiga chuma mbili dhidi ya Liverpool, Man United wakashinda 2-1 lakini Rashford hakuwa anapewa nafasi mara kwa mara.

Frank de Boer akizungumza kama mchambuzi kwenye TV alisema, ni bahati mbaya kwa Rashfor kuwa na kocha kama Mourinho kwasababu hafikirii kabisa kuwapa vijana nafasi zaidi ya kufikiria kushinda.

Rashford

Kumbuka Frank de Boer ni kocha lakini hakuwa na kazi wakati huo. Aliwahi kuifundisha Crystal Palace akafukuzwa baada ya wiki nne tu.

Mechi iliyofuata (baada ya ile ya Liverpool), Mourinho alikuwa na waandishi akiizungumzia hali ya timu yake. Ndipo aliamua kukumbusha maoni ya Frank de Boer.

Mourinho alisema, “Nilisoma mahali kuhusu kocha mbovu kuwahi kutokea kwenye historia ya premier league, ni yule Frank de Boer aliyesema sistahili kuwa kocha wa Marcus ”

Rashford

“Amecheza mechi saba, ana ushindi sifuri na mabao sifuri ya kufunga. Kama angekuwa kocha wa Rashford, Rashford angejifunza zaidi kupoteza mechi kuliko kushinda. Kwasababu yeye ni mtaalamu wa kupoteza mechi”


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa