BEKI wa kimataifa Hector Bellerin, wa Hispania anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona, amekubali kupunguza mshahara wake wa sasa kwa kiasi kikubwa ili aendelee kusalia klabuni hapo.

BEKI wa kimataifa wa Hispania anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona Hector Bellerin, amekubali kupunguza mshahara wake wa sasa kwa kiasi kikubwa ili aendelee kusalia Barcelona.

Bellerin amefikia uamuzi huo baada ya kuhitaji kusalia klabuni hapo, na uongozi wa Barcelona umempatia mkataba wa mwaka mmoja tu wenye masharti ya kuongeza pale utakapomaliza.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwandishi wa habari hususani za usajili Fabrizio Romano alisema kuwa, beki huyo alikataa ofa mbili kutoka vilabu vya Italia vilivyoonesha nia ya kuhitaji saini yake.

BEKI wa kimataifa wa Hispania anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona Hector Bellerin, amekubali kupunguza mshahara wake wa sasa kwa kiasi kikubwa ili aendelee kusalia Barcelona.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 27, alianza maisha yake ya soka Barcelona, ​​na akahamia Arsenal mwaka 2011. Tarehe 21 Novemba 2016, alitia saini mkataba wa muda mrefu uliomfunga Arsenal hadi 2023, lakini akarejea Barcelona Septemba 2022, baada ya kuutumia mwaka uliopita kwa mkopo akiwa na Real Betis.

Hector Bellerin Akubali Kukatwa Mshahara ili Kusalia Barca

Beki huyo aliichezea Timu ya Taifa ya Hispania mashindano ya vijana chini ya miaka 16 hadi chini ya 21. Alianza kwa mara ya kwanza timu ya taifa mwaka wa 2016 na baadaye akachaguliwa kwenye Mashindano ya Europa ya mwaka 2016.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa