Kinda wa Jamhuri ya Czech Adam Hlozek amesaini dili ya miaka mitano na klabu ya Bundesliga akiungana na mtaifa mwenzke Patrick Schick.

Bayer Leverskusen wanataka kukiimarisha kikosi chao baada ya kupata fursa ya kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kumaliza nne za juu katika ligi hivyo wameingia sokoni kutafuta wacheza ambao wataongeza nguvu.

Hlozek amesaini na Leverkusen akitokea klabu ya Sparta Prague ambako alifanikiwa kufunga mabao 34 kwenye michezo 105 ndani ya miaka minne.

Hlozek mwenye umri wa miaka 19 anaungana Schick ambaye pia ameongeza mkataba na miamba hao wa Ujerumani.

“Adam ni mchezaji ambaye anaweza kuwa tishio kama mshambuliaji wa pili au akiingia kama winga,” alielezea mkurugenzi wa michezo wa Leverkusen Simon Rolfes.

“Uwezo wake mwingi, nguvu na umaliziaji utatoa chaguo zaidi kwa mashambulizi yetu.”


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa