Hugo Lloris golikipa wa klabu ya Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya Ufaransa ameonesha kuhofia majeraha yaliyowapata nyota wa timu yake ya taifa Paul Pogba pamoja na Karim Benzema.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa amezungumza baada ya kuipatia timu yake kwenye ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Olympique Marseille wa bao mbili kwa bila na kusema anapata wasiwasi majeraha yanayowapata wachezaji wao muhimu kwenye kikosi kwani wanapahitaji kwenda Qatar mwezi Novemba wakiwa na wachezaji wao bora wote kikosini.

hugo llorisPaul Pogba yeye anaweza kukosekana kabisa kwenye michuano hiyo kwani mwanzo hakupanga kutibu kidonda chake kwenye goti kwa upasuaji lakini imelazimu kufanyiwa upasuaji kwenye goti lake jambo ambalo litamuweka nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.

Kwa upande mwingine Les Blues wamepata pigo jingine baada ya mshambuliaji wao wa kutumainiwa Karim Benzema kutolewa kwenye mchezo wa jumanne kwenye ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Celtic na kuarifiwa kua amepata jeraha kwenye nyama za paja ambvalo litamuweka nje kwa wiki kadhaa kitu kinachowafanya wafaransa na nahodha wao Lloris kupata shaka kutokana na majeraha yanayoandama nyota wao kikosini.

Timu ya taifa ya Ufaransa ambao ndo mabingwa watetezi wa michuano hiyo wana matumaini makubwa ya kwenda Qatar kutetea ubingwa wao walioutwaa mwaka 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Croatia.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa