Ibrahimovic Apona COVID-19 Kuelekea Milan Debi.

Zlatan Ibrahimovic yupo sawa baada ya kupima mara mbili na vipimo kuonesha hana maambukizi tena ya virusi vya Corona klabu yake ya AC Milan imethibitisha.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 39 alikutwa na maambukizi ya COVID-19 mwezi uliyopita na alilazimika kuikosa michezo minne kutokana na kujitenga ili kuepuka maambukizi zaidi.

Milan, ambao watawakabili Inter kwenye debi itakayo pigwa Oktoba 17 baada ya mapumziko kwaajili ya michezo ya kimataifa, imethibitisha Ibrahimovic kwa sasa yupo tayari kwaajili ya kucheza baada ya kumaliza muda wake wa kujitizamia.

Ibrahimovic Apona COVID-19 Kuelekea Milan Debi.
Straika, Zlatan Ibrahimovic.

“AC Milan inatangaza kwamba Zlatan Ibrahimovic amepimwa na kukutwa hana maambukizi baada ya kufanya zoezi la kupima mara mbili mfululizo,” Maelezo ya klabu yalisema.

“Mamlaka za Afya katika jiji la Milan zimekatisha siku zake za kukaa karantini.”

Mswideni huyo alisema lilikuwa ni jambo baya kwa virusi hivyo kumuandama yeye tu na baada ya kuwa sawa ametoa shukrani zake kupitia mitandao ya kijamii siku ya Ijuma.

“Umepona!” Zlatan aliandika kwenye mtandao wa Twitter.

“Mamlaka za afya zimenitaarifu kwamba muda wa kukaa karantini umeisha.

“Unaweza kwenda nje sasa.

Ibrahimovic ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na Milan baada ya kurejea katika klabu hiyo mwezi Januari.

Amefunga magoli matatu katika michezo miwili kwenye Serie A msimu huu kabla hajagundulika kuwa na maambukizi.


Weka Pesa kwa Airtel Money!

Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!

Soma Zaidi

30 Komentara

    afadhali maana tulikuwa tunahofia afya ya kiungo mahili

    Jibu

    Hii ni habari njema kwa Ac Milan

    Jibu

    Pole Sana Ibrahimovic.

    Jibu

    Hii Ni habari njema kwa mashabiki 👏👏

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki wa ac Milan na uwongozi kwa jumla

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Vizuri Sana Movic kwakurejea kwenye krabu yake kujiunga

    Jibu

    Mungu ni mwema atimae analejea kikosini

    Jibu

    Mungu ni mwem kila wakt

    Jibu

    Ibrahimovic anatakiwa kufikiria kuanza jukumu la kuwa kocha au Ukrugenzi wa michezo, umri umesogea mno#meridianbettz

    Jibu

    Duuuh ni hatari

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Safi sana pia sisi mashabiki tumepokea vizuri taarifa hizi

    Jibu

    habari njema hii

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Afazar anogeshe mechi

    Jibu

    Covid 19 imekua balaa

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki wake

    Jibu

    Cadabra inter watapata shida kweny derby hii

    Jibu

    MIlAN derby MAMBO ni MOTO

    Jibu

    Afadhali ,habari njema.

    Jibu

    Afadhali daah

    Jibu

    Bora

    Jibu

    Ni habari njema kwa mashabiki

    Jibu

    Mungu Ni mwema kwako hatime unarud tena kikosin

    Jibu

    Hii ni habari njema kwa ac millan

    Jibu

    Goodnews

    Jibu

    Mungu yu mwema

    Jibu

    Kila lakheri kwake

    Jibu

Acha ujumbe