CHAMA cha Soka wilaya ya Ilala (IDFA) kimetuma salamu kwa klabu ya Pan African inayoshiriki michuano ya Championship kuwa na upendo na mshikamano kwa ajili ya kutimiza malengo ya timu kwa msimu ujao.

Kikao cha wanachama na viongozi kimefanyika leo alhamis kwenye ukumbi wa Falcon Hotel uliopo Lumumba, Dar.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa IDFA, Daudi Kanuti amesema kuwa “Nimefurahi sana kuwaona wanachama waliojitokeza hapa kwa ajili ya mkutano huu wa leo.

“Kwa niaba ya Chama cha soka tunatoa wito kwamba muwe na umoja na ushirikiano katika kipindi hiki ambacho mnaelekea kwenye uchaguzi mkuu na kuijenga timu kwa msimu ujao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa