NYOTA wa zamani wa Yanga Deus Kaseke amefunguka kuwa wakati yupo kwenye timu hiyo alivumilia mengi ikiwemo kukosa muda mwingi wa kucheza kwenye siku zake za mwisho klabuni hapo.

Mchezaji huyo ambaye alidumu kwa takribani miaka   nane kwenye timu hiyo amesema uvumilivu na subra ilikuwa ni sehemu ya maisha yake kwenye timu hiyo na ni kitu ambacho ataendeleza akiwa na Big Stars.

 Kaseke alisema kitu kibaya kwa mchezaji ni kukosa muda wa kucheza kwenye timu na yeye alikutana nalo hilo akiwa na Yanga lakini hakuweza kukata tamaa alijipa moyo wa uvumilivu na subra hadi anaondoka kwenye timu hiyo.

“Ni kweli kuwa sikuwa napata muda wa kucheza nikiwa Yanga, nilivumilia hilo na mengine mengi kwa sababu nilijua ni sehemu ya maisha yangu ya mpira.

“Nitaendelea kuwa hivyo hadi kwenye timu yangu hii mpya ya Singida Big Stars na hata kama ikitokea nimeondoka hapa na kwenda sehemu nyingine,” alisema.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa