Ole Gunnar Solskjaer ameweka wazi kuwa kufanya kazi klabu ya Manchester United ndiyo kitu pekee ambacho amekuwa akihitaji kukifanya. Wakati nwake wote amekuwa akifikiria kuja kufanya kazi kama meneja wa Manchester United.
Bwana huyu ambaye alipewa umeneja wa mda mwishoni mwa mwaka uliopita, amewaongoza klabu hiyo kubadilisha kabisa matokeo mabaya waliyokuwa nayo wakiwa wanahangaikia kumaliza kwenye 4 bora kwenye msimamo wa Ligi ya Uingereza.
Solskjaer ambaye mpaka sasa ameshinda gemu 14 kati ya gemu 17 za klabu hiyo baada ya kuchukua jukumu la umeneja anasema kuwa alikuwa anafikiria kuwa anaweza kuwa meneja mzuri zaidi kuliko kuwa mchezaji.
Mkuu huyu anatajwa kuwa katika kipaumbele cha klabu hiyo kupewa umeneja wa kudumu klabuni hapo licha ya uongozi wa klabu hiyo kusisitiza kuwa haihitaji kufanya maamuzi ya nani atakuwa meneja wa kudumu mapema hivi.
Licha ya kutambua changamoto zote za kuwa mchezaji wa klabu hiyo, kwa kipindi cha miezi kdahaa tayari amekutana na changamoto za kuwa meneja na yupo tayari kuendelea kupambana vilivyo kwa sababu anapenda kuwa sehemu ya klabu inayofanya maamuzi.
Furahav
Ole namkubali sana.