UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa watacheza pira spana, pira kodi dhidi ya Simba kwenye mchezo ujao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Leo Septemba 7, KMC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery itamenyana na Simba inayonolewa na Seleman Matola ambaye ameachiwa mikoa ya Zoran Maki.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaokuwa na ushindani mkubwa.

“Tunakwenda kucheza na Simba na tunatambua kuwa utakuwa mchezo mgumu lakini tunakwenda kucheza pira spana, pira kodi pira mapato kwa wapinzani wetu.

“Tumefanya usajili mzuri na wachezaji wanajua kwamba tunahitaji kupata ushindi mechi mbili ambazo tumecheza pamoja na mechi za kirafiki zimezidi kutuimarisha,” amesema Christina.

KMC imekusanya pointi moja baada ya kucheza mechi mbili na Simba imekusanya pointi sita zote zikiwa zimecheza mechi mbili ambazo ni dakika 180.

KMC vs SIMBA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa