ALIYEKUWA kocha wa viungo wa Simba Mtunisia, Adel Zrane ameweka wazi kuwa anaamini uongozi wa Simba umejifunza mengi,  kwa kuwa na nyakati mbaya msimu ulioisha na anaamini watarejea kwa kishindo kurejesh hesghima yao, huku akiwaonya Yanga kutobweteka na mafanikio waliyopata msimu huu.

Simba wamemaliza vibaya msimu huu ambapo wamepoteza mataji yao yote matatu ambayo walishinda msimu uliopita na mataji hayo yamechukuliwa na mtani wao Yanga huku wao wakiambulia Kombe la Mapinduzi pekee.

Yanga wao wamemaliza msimu huu kwa mafanikio makubwa ambapo wamefanikiwa kushinda Kombe la Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho Afrika, huku pia wakiwa ni mabingwa wa Ngao ya Jamii.

Adel Zrane, Simba
Adel Zrane, Simba

Adel alisema: “Najua Simba wamekuwa kwenye wakati mgumu sana msimu huu, kupoteza makombe yao yote tena mbele ya Yanga ni jambo ambalo bila shaka litakuwa limewaumiza sana, lakini naamini wamejifunza na watarudi kwa kishindo msimu ujao ili kurejesha heshima yao.”

“Kwa upande wa Yanga bila shaka nawapongeza kwa mafanikio makubwa waliyoyapata, lakini mafanikio hayo yasiwafanye wakajisahau bali wajue wana kazi ngumu mbele yao ya kufanya mafanikio hayo kuwa endelevu.”

Zrane alidumu Simba kwa misimu minne kabla ya mwanzoni mwa mwaka huu kufutwa kazi sambamba na aliyekuwa kocha mkuu Didier Gomes.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa