Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Mbeya Kwanza MBWANA Makata na meneja wa timu hiyo David Naftari wamepunguziwa adhabu yao ya kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitano waliyopewa miezi michache iliyopita.

Taarifa ambayo iltolewa jana Julai 9,2022 imeweza kueleza kuhusu suala hilo la viongozi hao kupunguziwa adhabu. Awali ilibidi watumikie adhabu ya kutojihusisha na soka kwa muda wa miaka mitano na sasa itakuwa kwa miezi sita pekee.

Adhabu hiyo ilitokana na wao kukutwa na kosa la kukiuka sheria na kushinikiza timu yao kutocheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Namungo iliyokuwa imepangwa kuchezwa Mei 14 mwaka ambayo haikuchezwa.

Kutokana na mchezo huo kutochezwa Namungo walipata pointi tatu za mezani na mabao matatu.

Katika taarifa ya kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyotoka leo ikizingatia kikao cha Julai 6,2022 imeeleza Makata na Naftari wamepunguziwa adhabu kutokana na wawili hao kukiri makosa yao na kuomba radhi.

Makata ni moja ya makocha wakongwe ambapo aliibuka ndani ya Mbeya Kwanza baada ya kupigwa chini ndani ya kikosi cha Dodoma Jiji.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa