Kylian Mbappe Kutosaini Mkataba Mpya PSG

Nyota wa PSG, Kylian Mbappe ambaye aliwagharimu dau la paundi milioni 180 kwenye uhamisho ameweka wazi kuwa hatarajii kusaini mkataba mpya klabuni hapo.

Wakati tetesi za usajili zikipamba moto, haikudhaniwa kwa urahisi kuwa Kylian Mbappe angekuwa anatarajia uhamisho wa mapema klabuni hapo.

Staa huyu mwenye miaka 20, moja kati ya vijana machachali zaidi na wenye thamani katika ulimwengu wa soka alishawahi kuwa mchezaji wa Monaco.

MBappe amekuwa akifanya vyema sana kwenye ligi ya Ufaransa na kuwasaidia PSG kuendelea kuwa watabe kwenye Ligue 1. Alifunga magoli 60 kwennye mechi 87 msimu uliopita toka alipofika klabuni hapo.

Amekuwa msaada mkubwa kwa PSG kwenye ushambuliaji hasa kipindi ambacho Neymar alikuwa akiuguza majeraha yake.

Raisi wa klabu hii aliweka wazi kuwa hatarajii kumuuza staa huyu mapema msimu huu wa kiangazi. Alisistiza kuwa anahitaji wachezaji ambao watakuwa wakienda samaba ambao wapo tayari kufanya chochote kwa ajili ya klabu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chapisho la la Kihispania la Marca, inadaiwa kuwa Mbappe hana mpango wa kusaini mkataba mpya klabuni hapo. Jarida hililinasisitiza kuwa Mbappe hatafanya hivyo licha ya wingi wa pesa zinazoweza kuwekwa ili kumshawishi.

Lakini Kylian Mbappe bado ana mkataba wa miaka mitatu klabuni hapo wakati akiwa hafikirii kuongeza mda.

Real Madrid ni moja kati ya klabu zinazomwinda staa huyu.

2 Komentara

    Duuuh

    Jibu

    Mbappe angeenda madrid angepata mafanikio mengi.

    Jibu

Acha ujumbe