Raisi wa La Liga anashutumiwa kwa kukosa heshima na kumzushia nyota wa PSG Kylian Mbappe juu ya dili la staa huyo na klabu yake ya sasa.

Javier Tebas, Bosi wa Ligi ya Hispania alinukuliwa akisema suala la Mbappe kusaini mkataba mpya na PSG ni skendo na tusi kwa soka. Pia ilidaiwa kuwa La Liga waliwasilisha malalamiko kwa UEFA juu ya dili hilo wakitaja kuwa linatishia uchumi wa soka la Ulaya.

Bosi huyo wa La Liga alikuwa anafananisha nafasi ya Real Madrid kumnasa staa huyo bila kuchakachua suala la malipo yake, ukifananisha na fedha zilizowekezwa na PSG kuhakikisha wanasalia na staa huyu.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Ufaransa (LFP) bwana Vincent Labrune alimwandikia barua bosi huyo wa La Liga, barua ambayo iliwasilishwa na ajenti wa habari PA.

Barua hiyo ilielezea kutokubaliana kwao na kile wanachokiita shambulio la Ligue 1 na klabu yao kutoka Tebas.

“Kwa pamoja tumeshitushwa na kitendo cha shambulio kama hili, kwa nafasi uliyonayo kama Raisi wa Ligi za Ulaya, ambapo ulitakiwa kuwakilisha ligi zote za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ligue 1, na washirika wa Baraza la UEFA”

 

Sehemu ya barua ya Vincent Labrune

Kylian Mbappe Achagua Ligue 1 dhidi ya La Liga

Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa Tebas kuwazungumzia mastaa wakubwa na kuleta gumzo kwenye vichwa vya habari za michezo. Bwana huyu aliwahi pia kuwazungumzia Lionel Messi, Sergio Ramos na sasa Mbappe.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa