Ukiniuliza kwanini Frank Lampard msimu uliopita alifanya vema, nitakujibu kuwa, ni kwasababu wachezaji walikuwa wanamtumikia sana. Walikuwa wakimtazama kama ‘role model’ hakuna heshima nyingine ambayo wangeweza kumpa zaidi ya kujitoa kwa ajili yake.
Nakubali kuwa Chelsea ilikuwa inashinda kwa mbinu za Lampard lakini zaidi sana, Chelsea ilikuwa inashinda kwa ari, kujitoa (Spirit). Bahati mbaya ya kushinda kwa ari ni kuwa, timu inapodondora na kuanza kukosa matokeo, huwa inashuka na kupelekea kukosa ujasiri. Ili ari iendelee kuwepo unahitaji kuendelea kupata matokeo.
Unahitaji nini cha kukupa matokeo zaidi ya mbinu na wachezaji bora? Hakuna. Chelsea kwa sasa wana wachezaji bora. Wanachokosa ni hicho kingine, namna ya kuupata ubora wa wachezaji.
Kupata ubora wa mchezaji unamuhitaji mwalimu zaidi, kisha mchezaji. Mwalimu anaupata ubora wa mchezaji kwa kutengeneza timu ambayo itampa nafasi kila mchezaji kufanya majukumu ambayo yanakuwa bora na marahisi kwake.
Kwa mfano, Kai Haveirtz, si aina ya mtu anayeweza kuwa Mtumwa uwanjani akakimbia kilometa nyingi kuutafuta mpira, si aina ya mtu unayeweza kumtuma akazuie na akafanya vizuri. Ni mpiga pasi mzuri asiyependa bugudha, hivo kama kocha unaitengeneza timu itakayokuwa na watumwa na wafukuza mpira, halafu yeye anafanya kazi yake anayoiweza
Kitu kama hicho unakifanya kwa timu nzima. Wale unaoamua wawe watumwa wanaondoka kwenye majukumu mengine. Inawezekana ukamlazimisha mchezaji kufanya jukumu asiloliweza, lakini unamtengenezea mazingira ambayo atafanya majukumu anayoyaweza zaidi. Labda hiko ndicho kitu anachokikosa Lamps.
Kitu kingine anachokikosa Lampard, ni uvumilivu na kutokujua kipi kinamfaa zaidi. Unajua tofauti na ukuta, labda na Mason Mount katikati ya kiwanja, hakuna wachezaji wengine unaoweza kuwataja kama sehemu ya kikosi cha kwanza cha Chelsea. Lampard anabadilika kila siku.
Ukifanya vizuri ukitokea benchi, basi mechi ijayo unaanza. Uki’flop’ mechi hii, mechi ijayo haupati nafasi. Sijui ukocha lakini, hauwezi kupata muunganiko kwa staili hii.
Kitu pekee ninachoamini ni kuwa, Lampard bado ana nafasi ya kufanya vizuri. Ni kocha mchanga mwenye muda mrefu wa kujifunza.
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.
Lydia Emmanuel Magoti
Nikweli kabisa
Adelta
Lampard ni kocha ambaye bado anamda wa kujifunza
Magdalena
Lampard ni kocha mzuri Sana tu na Chelsea watamkumbuka
Rahma
Habari njeam
Caroline
Lampard alikua na msimu mzuri Sana msimu uliopita
Khadija
Habari njema
Dorophina
Lampard akatafute kambi sehemu nyingine kocha mzuri tu
Venerose
Good news
Ernest Kimeru
Wachezaji wa Chelsea wameshindwa kumsoma Lampard
David Pere
Kitu kingine anachokikosa Lampard, ni uvumilivu na kutokujua kipi kinamfaa zaidi. Unajua tofauti na ukuta, labda na Mason Mount katikati ya kiwanja, hakuna wachezaji wengine unaoweza kuwataja kama sehemu ya kikosi cha kwanza cha Chelsea. Lampard anabadilika kila siku.
Issa
Chelsea mliwah mno
Hopemwaikuka
Inawezekana pia
Sarah
Habari nzuri
warda
ndo ajifunze
Sadick
Lampard alitakiwa kupata muda zaidi wa kujifunza na kufundisha timu kubwa kama Chelsea.