Mshambuliaji wa timu ya Barcelona Robert Lewandowski amepiga hattrick yake ya kwanza akiwa Nou Camp huku akiwa ndio mchezaji wa kwanza kupiga hattrick katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Lewandowski Apiga Hattrick UEFA

Lewandowski amefunga mabao hayo matatu dhidi ya Viktoria Plizen  na mawili yakifungwa na Kessie pamoja na Torres, huku akiwa ndiye mchezaji pekee kupiga hattrick akiwa na timu tatu tofauti. Alifanya hivyo akiwa na Borrusia Dortmund, Bayern Munchen na sasa akiwa Barcelona. Barca wamefunga jumla ya mabao matano na wakati kwa Viktoria bao lao la kujifutia machozi lilifungwa na  Sykora na mchezo kumalizika kwa mabao 5-1.

Lewandowski  mpaka sasa amecheza jumla ya michezo mitano na akifunga mabao nane katika mashindano yote kwenye Laliga pamoja na michuano hii ya UEFA ambayo imeanza 6 September.

 

Lewandowski Apiga Hattrick UEFA

Mchezo unaofata Barcelona atakutana na miamba ya Ujerumani Bayern Munchen ambao nao wameanza vizuri michuano hii ambapo mechi yao ya kwanza wameshinda kwa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Intermillan.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa