Luis Enrique Amkingia Kifua Winga Ansu Fati.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Spain Luis Enrique amemtetea mchezaji Ansu Fati baada ya kupambana sana kwenye mchezo wa Nations League dhidi ya Switzerland ambapo Hispania iliibuka na ushindi wa 1-0.

Kinda huyo wa miaka 17 ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Barcelona na mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga katika taifa hilo, alicheza dakika 57 kabla nafasi yake haijachukuliwa na nyota wa Wolves Adama Traore.

Fati alishindwa kutumia vyema nafasi mbili za mwanzo kwenye mchezo huo, na alifanikiwa kupiga shuti moja na hakutengeneza nafasi yoyote ya kufunga kwa wachezaji wenzake.

Lakini pia alishindwa kupiga cross na mfumo wa 3-5-2 wa Switzerland ulidhihirisha kumbana wakati Silvan Wilder na Nico Elvedi walipelekea ugumu kwa upande wa kushoto wa Spain.

Luis Enrique Amkingia Kifua Winga Ansu Fati.
Winga wa Spain, Ansu Fati.

“Kukabwa mara nyingi limekuwa ni tatizo kwa Ansu Fati na kila mshambuliaji,” Luis Enrique alisema siku ya Jumatatu ikiwa Spain wanajiandaa kuwakabili Ukraine.

“Malengo yetu ni kutengeneza faida nyingi kwa washambuliaji wetu baada ya hapo kila gemu itakuwa hivyo.

Safu ya ushambuliaji ya Spain pia ilishindwa kufanya maajabu baada ya kwendsa sare ya 0-0 na Portugal wiki iliyopita, lakini safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Kombe la Dunia 2010 inaonekana kuimarika.

Katika michezo 15 ambayo hawajafungwa tangu mwaka 2018, La Roja wameruhusu magoli sita pekee na kuapata clean sheet nane.

Luis Enrique anafurahi kuona wachezaji kama Pau Torres, Eric Garcia na Diego Llorente wakicheza vizuri na anamaamini wachezaji wenye umri mdogo wanaweza wakamsaidia nahodha Sergio Ramos kuimarika.


Unapenda kuwa shujaa?

Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua. 

Cheza sasa 

Samurai Ken Online Casino

26 Komentara

    Ansu fat ni kinda ataeibeba Spain kwa muda

    Jibu

    Ansu fat ni mchezaji chipukizi anayekuja kwa speed

    Jibu

    Ansu fati anahitaj muda co kpnd hch kumtengenezea zongo juu ya kiwango chake

    Jibu

    Ansu yuko vizuri acha akingiwe kifua maana atafanya mengi sana kwani hata umri wake unaridhisha

    Jibu

    Fat ni mchezaj ambae kiwango chake kitaimarika kadri atakavyopata mechi zaid

    Jibu

    Hakua na kiwango kizur

    Jibu

    Ansu fundi sina mashaka nae

    Jibu

    Yuko vizuri sana

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Kiwango chake hakiridhishi

    Jibu

    Yupo vizur

    Jibu

    ansu fati ni mpole sana na mkarimu ndo maana ata kocha wake kaamua kumkingia kifua

    Jibu

    Huyu dogo yuko vizuri

    Jibu

    Wampe mda tu ansu fati ni mchezaji chipukizi hanaye jituma sana

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Yuko vzr sana

    Jibu

    Ansu ni mchezaji mzuri anachotakiwa kwa sasa ni kupewa mda tu

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Fati anahitaji muda zaidi

    Jibu

    Ansu fati anahitaji muda zaidi

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Saf

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Ansu fat ni mchezaji chipukizi anayekuja vizur

    Jibu

    Gud

    Jibu

Acha ujumbe