Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuwa wamepewa nafasi ya kumsajili winga wa Real Madrid Marco Asensio msimu huu wa joto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, akiwa anakaribia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake, ni mmoja wa wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza ambao hawana uhakika na mustakabali wao Santiago Bernabeu.

Asensio amefunga mabao 12 na kutoa pasi asisti 2 kwenye mechi 42 alizoichezea Real Madrid msimu ulioisha wa 2021-22, lakini winga huyo hapewi nafasi ya uhakika ya kuanza chini ya Carlo Ancelotti.

Kwa mujibu wa El Chiringuito TV kupitia gazeti la The Mirror, Asensio amepewa ofa ya kwenda Man United na wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Kocha wa Man United Erik ten Hag anatazamiwa kufanya mabadiliko ya jumla kwenye kikosi chake cha kwanza msimu huu hasa katika safu ya kiungo, kufuatia kuondoka kwa Paul Pogba, Jesse Lingard, Juan Mata na Nemanja Matic.

Man United Wana Mpango Gani na Marco Asensio?

Asensio, ambaye amekuwa na Real Madrid tangu 2015, amewahi kuhusishwa na vilabu vya Arsenal, Tottenham Hotspur na AC Milan.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa